Mh. Joseph Mbilinyi (SUGU) Amwakikishia Spika wa Bunge Mh. anne Makinda kwamba mafisadi wote ni lazima wang'oke.
Mbilinyi "Sugu" amwambia Spika "nakuhakikishia upepo huu wa kimbunga lazima utawang'oa watake wasitake... Sitanii, kama hautang'oa nyumba utaondoka na paa..." Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Joseph Mbilinyi, amesema Mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete wanaotamba kuwa hawatang'oka kwenye wadhifa huo, watang'olewa kwa kimbunga kinachokuja. Akizungunza Mbunge Mjini Dodoma saa 6:45 mchana leo, amemhakikishia Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda kuwa moto uliowashwa na wabunge bila kujali itikadi zao kisiasa, lazima mawaziri waliotajwa kuhusika katika kashifa ya ubadhirifu watangoka. Amesema hata kama kimbunga hicho hakitang'oa nyumba nzima,lakini kitaondoka na paa la nyumba hiyo, akimwaanisha kuwa iwapo mawaziri hao wataendelea kung'ang'ania nyadhifa hizo, Waziri Mkuu Pinda atang'olewa kwa upepo huo. "Sitanii, huu ni upepo wa kimbunga, kam...