Posts

Showing posts from February, 2017

RAIS MAGUFULI AMTUMBUA FLORENCE MWANRI

Image
Tumbua Tumbua ya JPM Yarudi Tena,Safari Hii Amemtum,bua Kigogo Huyu wa Wizara ya Fedha..!!! Rais John Magufuli amemsimamisha kazi Kaimu Katibu wa Tume ya Mipango (Wizara ya Fedha), Florence Mwanri aliyeidhinisha kuanza kwa awamu ya pili ya ujenzi wa jengo jipya la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) (Terminal 3) kabla ya kumalizika kwa awamu ya kwanza. Rais Magufuli alifikia uamuzi huo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika mradi wa ujenzi wa jengo jipya na kuagiza shughuli za ujenzi wa uwanja huo ziendelee kuanzia leo. Katika ziara aliyoifanya jana ilielezwa kuwa mkandarasi anayejenga uwanja huo,  kampuni ya BAM International alitangaza kusitisha ujenzi kuanzia jana kutokana na kutolipwa madai yake. Hata hivyo, Rais Magufuli ameahidi kulipa fedha hizo haraka. Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa ilieleza kuwa Rais Magufuli alisikitishwa na namna mradi huo unavyotekelezwa, ikiwamo Serikali kukubali

Rais Magufuli asikitishwa na gharama ya ujenzi, uwanja wa ndege

Image
8 Februari 2017 Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha IKULU, TANZANIA Image caption Rais Magufuli asikitishwa na gharama kubwa ya ujenzi wa jengo la uwanja wa ndege Rais wa Jamhuri ya Tanzania John Pombe Magufuli, ameelezea kusitikishwa kwake na gharama kubwa ya ujenzi wa jengo jipya kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Gharama hiyo ni ya shilingi bilioni 590, ambayo ni kubwa ikilinganisha na jengo lililojengwa. Rais Magufuli amesema hayo alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye uwanja huo. "Hivi kulikuwa na sababu gani za nyinyi wataalamu wa serikali kukubali gharama kubwa namna hii, hivi hili jengo linafanana na bilioni 560," aliuliza Dkt. Magufuli. Awali mkandarasi anayejenga uwanja huo ambaye ni kampuni ya BAM International , alitangaza kusitisha ujenzi huo kutokana na kutolipwa. Mheshimiwa Rais Magufuli aliahidi kulipa fedha hizo. Kufuatia hali hiyo Mheshimiwa Rais mafufuli amemuagiza waziri wa u

Makonda aitwa bungeni kujieleza WEDNESDAY , 8TH FEB , 2017 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kauli moja limewaita mbele ya Kamati yake ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, na DC wa Arumeru Alexander Mnyeti kwa madai ya kudharau Bunge.

Image
Maamuzi hayo ni sehemu ya maazimio manne ya  Bunge yaliyopishwa usiku huu dhidi ya viongozi wanaoteuliwa na Rais hasa wakuu wa mikoa na wilaya, ambapo azimio lingine ni kumtaka Waziri wa TAMISEMI kutoa maelekezo kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kutoingilia majukumu yasiyo yao. Hatua hiyo inafuatia hoja iliyotolewa bungeni hapo na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara, kufuatia kauli inayodaiwa kutolewa na Mkuu wa Mkoa wa  Dar es Salaam Paul Makonda inayodaiwa kuwa ni dharau kwa Bunge. Pia Mwita amedai kuwa viongozi mbalimbali hasa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wamekuwa wakitumia madaraka yao vibaya kiasi cha kuingilia majukumu yasiyo yao, na wakati mwingine kuingilia majukumu ya Bunge, na kutolea mfano Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Alexander Mnyeti.   Baada ya hoja yake kukubaliwa na Mwenyekiti wa kikao hicho Mh Andrew Chenge, wabunge wameijadili ambapo wabunge kadhaa akiwemo Ester Bulaya, Zitto Kabwe,

M.M.I STEEL MILLS WAKANUSHA KUHUSIKA NA MADAWA YA KILEVYA

Image

BREAKING NEWS: Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji, mbunge wa zamani wa Kinondoni Iddy Azzan na Askofu Gwajima ni miongoni mwa watu 65 waliotajwa kwenye awamu ya pili ya vita dhidi ya madawa ya kulevya na wanatakiwa kuripoti Kituo kikuu cha Polisi, Ijumaa saa tano asubuhi. #Namuunga mkono Paul C. Makonda#

Image

MOHAMMED HABIBU MNYAA AFUKUZWA UANACHAMA CUF

THE CIVIC UNITED FRONT (CUF –Chama Cha Wananchi) TAARIFA KWA UMMA Imetolewa leo Tarehe 7/2/2017 MOHAMED HABIBU MNYAA AFUKUZWA UANACHAMA Leo tarehe 7/2/2017 Mkutano Mkuu wa Tawi la Chanjaani, Jimbo la Mkoani wilaya ya Mkoani-Pemba, umefanya maamuzi ya kumfukuza uanachama wa CUF Mohamed Habibu Mnyaa  kutokana na kukiuka katiba ya chama Ibara ya 12 (6)(7)(16) kutokana na kuwa na mwenendo usiofaa wa kuwagawa wanachama, kueneza taarifa za upotoshaji dhidi ya viongozi na Chama, kufanya vitendo vya hujuma za kutaka kukidhoofisha Chama, kudharau na kushindwa kuhudhuria na kutoa ushirikiano kwa tawi lake kila alipotakiwa kufanya hivyo. Mkutano Mkuu wetu wa leo umehudhuriwa na wajumbe halali 112 kati ya wajumbe wote halali 113. Wajumbe wote 112 wamepiga kura za ndio kuazimia kumfukuza uanachama kwa mujibu na mamlaka ya kikatiba yaliyoelezwa katika katiba ya CUF ukurasa wa 29 ibara ya 18(1)(ix) kuhusu wajibu wa Mkutano Mkuu wa Tawi kama ilivyoeleza kuwa;  “Kumchukulia hatua za nidhamu

RAIS MAGUFULI AMTEUA MKUU MPYA WA MAJESHI TANZANIA.

Magufuli amteua mkuu mpya wa majeshi Tanzania Mkuu mpya wa majeshi nchini Tanzania Jenerali Venance Mabeyo Rais John Pombe Magufuli amemteua Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa mkuu wa majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania akichukua mahala pake jenerali Davis Mwamunyange aliyestaafu. Taarifa kutoka ikulu iliotumwa katika vyombo vya habari inasema kuwa Luteni huyo sasa amepandishwa cheo na kuwa jenerali kamili. Wakati huohuo rais amemteua meja jenerali James Mwakibolwa kuwa mnadhimu mkuu wa majeshi ya ulinzi akichukua mahala pake Jenerali Mabeyo.Pia yeye alipandishwa cheo cha luteni jenerali. Rais amesema kuwa uteuzi huo unaanza kutekelezwa mara moja. Tarehe ya kuapishwa kwa wawili hao itatangazwa baadaye.