Maisha yetu ni bora kuliko kazi na vyeo vyao...
Na Msafiri wa Yowa II Jr.
Katika nchi yetu Kuchukua sheria mkononi kwa Askari au Raia wa kawaida si kitu cha ajabu sana, aidha kutokana na vyeo vyao na nafasi walizonazo Serikalini. Imefikia hatua hata polisi wamefanya mauaji kwa raia wasio na hatia kwa tamaa za mali ambao ni sawa na uporajiu wizi na hakukuwa na mtu mwingine yoyote yule wa kukemea unyama huo.Sasa kama anaelinda raia na mali nae ni mwizi sasa tumwamini nani? Mfano ni mauaji ya wafanyabiashara wa Morogoro maeneo ya msitu wa pande ambapo tumeona mpaka viongozi wa jeshi la polisi walishiriki kwa namna moja au nyingine.Polisi ndio wamekuwa wahalifu namba moja badala ya kuwa walinzi wa mali zetu na sisi wenyewe. Raia tumekuwa watumwa ndani ya nchi yetu kutokana na tamaa za baadhi ya viongozi wetu ambao hawajui misingi na kanuni za uongozi bali wameweka mbele uchu, uroho na ufisadi. Sitaki kuamini kama hawa viongozi na askari wanaofanya unyanyasaji kwa raia hawaamini kama mungu yupo na iko siku atawaadhibu kwa kile wanachokifanya...
Duniani pamekuwa si sehamu salama tena pa kuishi kutokana na tamaa za baadhi ya wachache, Mimi nitaendelea kuwalaani hawa viongozi wetu maamuma kwa huu upuuzi wanaoufanya kwa sisi raia kwani wao ndio wanaidhinisha huu upuuzi kwa kukaa kimya bila kukemea. Serikali kimekuwa chombo cha kuficha huu uovu wote na kuchekelea bila kukemea kwa sababu tu hawa wanaofanya huu unyama aidha ni ndugu zao au wanaujamaa au mabibi zao na hata washkaji zao.
Iko siku raia tutachoka na tutadai haki zetu hata kwa NGUVU.
Comments