Rais Magufuli asikitishwa na gharama ya ujenzi, uwanja wa ndege


  • 8 Februari 2017

Rais Magufuli asikitishwa na gharama kubwa ya ujenzi wa jengo la uwanja wa ndegeHaki miliki ya pichaIKULU, TANZANIA
Image captionRais Magufuli asikitishwa na gharama kubwa ya ujenzi wa jengo la uwanja wa ndege

Rais wa Jamhuri ya Tanzania John Pombe Magufuli, ameelezea kusitikishwa kwake na gharama kubwa ya ujenzi wa jengo jipya kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Gharama hiyo ni ya shilingi bilioni 590, ambayo ni kubwa ikilinganisha na jengo lililojengwa. Rais Magufuli amesema hayo alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye uwanja huo.
"Hivi kulikuwa na sababu gani za nyinyi wataalamu wa serikali kukubali gharama kubwa namna hii, hivi hili jengo linafanana na bilioni 560," aliuliza Dkt. Magufuli.
Awali mkandarasi anayejenga uwanja huo ambaye ni kampuni ya BAM International , alitangaza kusitisha ujenzi huo kutokana na kutolipwa. Mheshimiwa Rais Magufuli aliahidi kulipa fedha hizo.
Kufuatia hali hiyo Mheshimiwa Rais mafufuli amemuagiza waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mheshimiwa Prof Makame Mnyaa aliyeongoza nae kuunda timu ya wataalamu watakaofanya tathimini ya utekelezaji wa mradi huo, ikiwa ni pamoja na kuzungumza na mkandarasi anayejenga uwanja huo na Mhandisi mshauri ambao wamekubali kupunguza gharama za ujenzi wa mradi huo.

Comments

Popular posts from this blog

Secret Masonic Handshakes, Passwords, Grips And Signs Of Blue Lodge Masonry

ALAMA ZA FREEMASON.