Rais wa zamani wa Argentina Cristina Fernandez amefunguliwa mashtaka mapya ya ubadhirifu wa pesa



Rais wa zamani wa Argentina Cristina Fernandez amenguliwa mashtaka mapya ya ubadhirifu wa pesaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRais wa zamani wa Argentina Cristina Fernandez amenguliwa mashtaka mapya ya ubadhirifu wa pesa

Jaji mmoja nchini Argentina amemfungulia aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Cristina Fernandez de Kirchner na wanawe wawili mashtaka ya ubadhirifu wa fedha, na ufisadi.
Washiriki wake Fernandez wawili wa kibiashara pia wametajwa katika kesi hiyo na wote watano wamezuiliwa kuondoka Argentina.
Fernandez, mwenye umri wa miaka 64 tayari anakumbwa na mashtaka mengine ikiwemo kutumia pesa za serikali kiholela.
Amekanusha madai haya akisema kuwa ni vita vya kisiasa.
Katika taarifa siku ya Jumanne, maafisa walisema hakimu wa mahakama kuu Claudio Bonadio aliwasilisha rasmi ombi la kumfungulia Fernandes mashtka ya ubadhirifu wa fedha.
Mwanawe wa kike, Florencia, na wa kiume, Maximo pamoja na wanabiashara Christobal Lopez na Lazaro Baez pia wameshtakiwa.
Kulingana na taarifa hiyo, takriban dola milioni nane mali ya Fernandez imezuiliwa .
Mwezi jana, jaji mmoja aliamua kuwa Fernandez, aliyekuwa rais kutoka mwaka 2007 hadi 2015 ajibu shtaka la utumizi mbaya wa fedha akiwa ofisini.
Anadaiwa kuiamuru benki kuu kuuza dola kwa bei ya chini sana, wakati ambapo ilitarajiwa thamani ya pesa itashuka
Fernandez pia anakumbwa na shtaka tofauti la ufisadi ambapo inadaiwa serikali yake ilimpa mwanabiashara mmoja kwa jina Baez, ambaye ana uhusiano wa karibu na familia ya Fernandez, mikataba bila ya kufuatilia sheria zinazofaa.
Anadai mashtaka yote dhidi yake ni njia ya Rais nchi hiyo Mauricio Macri kumdhalilisha kisiasa.

Comments

Popular posts from this blog

Secret Masonic Handshakes, Passwords, Grips And Signs Of Blue Lodge Masonry

ALAMA ZA FREEMASON.