Mgawanyiko wa hisia kufuatia mashambulio ya Trump dhidi ya Syria
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Kombora kutoka kwenye meli za kijeshi za Marekani katika bahari ya Mediterranea Kumekuwa na shutuma na uungwaji mkono wa makombora iliyofyetuwa Marekani dhidi ya Syria. Inategemea ni upande upi wa mzozo huo mataifa yanaunga mkono. Mataifa yanayo unga waasi wanaopambana na utawala wa rais wa Syria Bashar al Assad, yameunga mkono shambulio hilo. Haki miliki ya picha AFP Image caption Baadhi ya watoto walioathirika na kemikali,Syria Uturuki imepokea vizuri ufyetuaji makombora hayo, wakati afisa wa wizara ya mambo ya nje wa Saudia amemsifu rais Trump kwa ukakamavu wake na Uingereza imejitolea usaidizi kikamilifu. Waziri mkuu wa Israel amesema ujumbe wa wazi umetumwa unaopaswa kusikika sio tu Damascus lakini pia Iran na Korea kaskazini. Kwa upande wake Iran ambayo kama Urusi inaunga mkono serikali ya Syria imeshutumu shambulio hilo. Haki miliki ya picha EPA Image caption Serikali ya Putin anasema kiongozi huyo am...