OMBI LA LULU LAKATALIWA
Msanii wa filamu za maigizo nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, leo amepandishwa tena kizimbani mara ya tatu katika kesi ya mauaji ya Kanumba inayomkabili ambapo mawakili wanaomtetea wakiongozwa na Kennedy Fungamtama waliwasilisha ombi la kurekebisha umri wa mshitakiwa huyo kuwa miaka 17 na si 18 kama ilivyowasilishwa mahakamani hapo.
Fungamtama na jopo lake walisema mteja wao ni mtoto mdogo hivyo kesi hiyo ipelekwe mahakama ya watoto na kuwasilisha cheti kinachoonesha ana umri wa miaka 17. Upande wa mashitaka umetupilia mbali ombi hilo na kudai cheti kilichowasilishwa kina mapungufu kadhaa likiwemo jina la Dyana ambalo halijawahi kusikika likitumiwa na mshitakiwa huyo.
Comments