Google kuwarudisha wafanyikazi kufuatia agizo la Trump

  • 28 Januari 2017

Kampuni ya Google imewataka wafanyikazi wanaofanya kazi katika mataifa ya kigeni kurudi nchini Marekani kufuatia agizo la rais wa taifa hilo Donald Trump
Image captionKampuni ya Google imewataka wafanyikazi wanaofanya kazi katika mataifa ya kigeni kurudi nchini Marekani kufuatia agizo la rais wa taifa hilo Donald Trump

Kampuni ya Google imewataka wafanyikazi wanaofanya kazi katika mataifa ya kigeni kurudi nchini Marekani kufuatia agizo la rais wa taifa hilo Donald Trump kuwazuia raia wa mataifa sitaya Kiislamu kuingia nchini humo.
Wahamiaji wa Syria wamepigwa marufuku kuingia nchini humo itakapotolewa ilani nyengine.
Visa za raia wa mataifa sita ikiwemo Iran na Iraq hazitatolewa kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo.
Googole imeambia BBC ina wasiwasi kuhusu agizo hilo na mikakati ambayo huenda ikawazuia watu wenye vipaji kuingia nchini Marekani.
Mwandishi wa BBC aneyesimamia maswala ya kibiashara Joe Lyam anasema kuwa agizo hilo la Donald Trump lina maana kwamba maelfu ya raia wa Iran,Iraq, Yemen, Suria,Somali na Libya hataruhusiwa kupanda ndege zinazoelekea Marekani hata iwapo wanamiliki Green Card.
Bw Trump amesema kuwa hatua hiyo itawazuia magaidi kutoingia nchini humo.
Lakini makundi ya haki za kibinaadamu yanasema kuwa hakuna ushirikiano kati ya wakimbizi wa Syria nchini Marekani na ugaidi.

Comments

Popular posts from this blog

Secret Masonic Handshakes, Passwords, Grips And Signs Of Blue Lodge Masonry

ALAMA ZA FREEMASON.