Rasmi: Ulimwengu asaini miaka mitatu sweden..
Klabu ya AFC Eskilstuna ya Ligi Kuu Sweden imethibitisha kuingia mkataba wa miaka mitatu na mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu.
Kupitia mtandao wa klabu hio, Ulimwengu ataichezea Eskilstuna kwa misimu mitatu baada ya kumwaga wino leo.
Ulimwengu amejiunga na timu hiyo kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka mitano na mabingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika, TP Mazembe.
Comments