Yahya Jammeh amekimbia nchi muda huu na kwenda pasipo julikana,Nchi za Afrika Magharibi zimesimamisha kwa muda operesheni ya kijeshi



_92805045_jammeh
Taarifa zinaelezwa kuwa Bw.Jameh ametoweka pasipo julikana ni baada ya kupewa muda mchache kuachia madaraka.
Nchi za Afrika Magharibi zimesimamisha kwa muda operesheni ya kijeshi nchini Gambia ili kuruhusu juhudi za upatanishi kufanyika katika kuutatua mgogoro wa kisiasa nchini humo.
Hata hivyo, afisa mmoja alielezwa kuwa operesheni hiyo ingeaza leo mchana iwapo Yahya Jammeh atakataa kukabidhi mamlaka kwa rais mpya, Adama Barrow, aliyeapishwa rasmi hapo jana kwenye ubalozi wa Gambia nchini Senegal.
Wakati huo huo televisheni ya taifa ya Gambia imearifu kwamba ujumbe wa viongozi wa nchi za Afrika magharibi ikiwa pamoja na marais wa Liberia Mauritania na Guniea wanatarajiwa kuwasili nchini humo leo ili kuendeleza juhudi za upatanishi.
Wakati hayo yakijiri wakuu wa jeshi na polisi wamesema kwamba hawatazifuata amri za Yahaya Jammeh huku kukiwa na taarifa kwamba Makamu wa Rais wa Gambia, Isatou Njie Saidy, amejiuzulu.
Mgogoro wa kisiasa nchini humo umesababishwa na hatua ya rais wa hapo awali Jammeh aliyeshindwa katika uchaguzi na kukataa kuachia madaraka kwa mpinzani wake Adama Barrow

Comments

Popular posts from this blog

Secret Masonic Handshakes, Passwords, Grips And Signs Of Blue Lodge Masonry

ALAMA ZA FREEMASON.