Mara saba Barack Obama alipotokwa na machozi

Mara saba Barack Obama alipotokwa na machozi

  • 12 Januari 2017


Obama atokwa na machozi akimshukuru Michelle

Rais wa Marekani anayeondoka Barack Obama alitokwa na machozi alipokuwa akitoa hotuba yake ya mwisho rasmi kama rais mjini Chicago.
Alitokwa na machozi alipokuwa anamshukuru mkewe Michelle pamoja na mabinti wao Malia na Sasha.
"Umeifanya ikulu ya White House kuwa pahala pa kila mtu," alisema kumhusu Michelle.
"Na kizazi kipya sasa kina malengo ya juu kwa kuwa umekuwa mfano mwema kwao."
Wakati wa utawala wake, alianzisha huduma ya bima ya afya na akarasmisha ndoa za wapenzi wa jinsia moja, lakini alisema mabinti wake ndio ufanisi wake mkubwa zaidi.
"Miongoni mwa yote niliyoyafanya maishani, ninajivunia zaidi kuwa baba yenu," alisema.
Haya hapa ni baadhi ya matukio ambayo yalimfanya Obama kutokwa na machozi alipokuwa rais.

Kifo cha bibi yake


Barack ObamaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBarack Obama alimsifu sana bibi yake aliyefariki siku za mwisho mwisho za kampeni yake ya urais 2008

Bibi yake Barack Obama, Madelyn Dunham, alifariki kutokana na saratani Novemba 3, 2008, siku ya mwisho ya kampeni yake ya urais.
Alitoa hotuba na kumsifu sana katika chuo kikuu cha North Carolina.
"Amekwenda nyumbani," alisema kabla ya kuwaambia watu waliohudhuria mkutano huo kwamba ilikuwa vigumu kwake kuzungumzia kifo cha bibi yake.
Kifo cha Dorothy Height

Barack na Michelle ObamaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBarack na Michelle Obama walihudhuria mazishi ya Height 2010

Dorothy Height alifahamika kama "Mlezi wa watetezi wa haki za kiraia Marekani" na aliandamana wakati mmoja na Martin Luther King Jr.
Dorothy alifariki mwaka 2010 akiwa na miaka 98. Alikuwa bado anatetea haki za kiraia hata akiwa mzee.
Na alikuwa kwenye jukwaa wakati wa sherehe ya kuapishwa kwa Obama mwaka 2009.
Mauaji shule ya Sandy Hook

Barack ObamaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBaada ya mauaji Sandy Hook, Obama aliongoza kampeni ya kurekebishwa kwa sheria za umiliki silaha

Watoto 20, wa umri wa kati ya miaka sita na saba, pamoja na walimu wao sita, waliuawa kwa kupigwa risasi na Adam Lanza mwaka 2012 katika shule ya Sandy Hook.
"Ninaweza tu kutumai kwamba intawasaidia kujua kwamba hamko peke yetu katika maombolezi haya," alisema kwenye hotuba baada ya shambulio hilo.
"Tumeomboleza nanyi, tumewakumbatia watoto wetu."
Mazishi ya Daniel Inouye

Barack Obama na Joe BidenHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBarack Obama alihudhuria mazishi ya Daniel Inouye akiwa na makamu wa rais Joe Biden

Daniel Inouye alikuwa seneta wa Marekani kutoka Hawaii kwa miaka 49, kati ya 1963 na 2012.
Barack Obama alizaliwa Hawaii na baada ya kifo cha Inouye, alisema alihamasishwa sana na mwanasiasa huyo Mmarekani wa asili ya Asia kuingia katika siasa.
"Jinsi alivyoheshimiwa katika taifa hilo, nafikiri kulinipatia kidokezo ya yale ambayo ningefanikiwa kutimiza maishani," Obama alisema 2012.
Wimbo wa Aretha Franklin

Barack na Michelle ObamaHaki miliki ya pichaCBS
Image captionBarack alitokwa na machozi Aretha Franklin alipoimba wimbo Natural Woman

Barack na Michelle Obama walikuwa wageni hafla ya kumkumbuka mtunzi wa nyimbo Carole King mjini Washington mwaka 2015 pale Aretha Franklin alipoimba wimbo wa (You Make Me Feel Like) A Natural Woman.
Mwanamuziki huyo wa miaka 74 aliuimba wimbo huo vyema na kwa njia iliyowagusa wengi.
Video ya Obama akitokwa na machozi iliyopeperushwa na CBS imetazamwa mara milioni kadha katika YouTube.

Sheria mpya za umiliki bunduki Marekani


Barack ObamaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBarack Obama aliwakumbusha watu kisa cha Sandy Hook alipowasilisha sheria mpya za umiliki wa silaha mapema mwaka 2016

"Kila wakati ninapowafikiria watoto hawa, huwa napatwa na kichaa," Barack Obama alisema kuhusu watoto waliouawa shule ya Sandyhook alipokuwa anawasilisha sheria mpya kuhusu umiliki wa silaha Marekani mapema Januari 2016.
Aliambia BBC mwaka 2015 kwamba kushindwa kwake kupitisha sheria hizo Marekani lilikuwa jambo lililomtatiza sana katika kipindi chake cha uongozi.
Juhudi zake za kubadilisha sheria hizo zimekuwa zikipindwa kila mara na chama cha Republican.

Comments

Popular posts from this blog

Secret Masonic Handshakes, Passwords, Grips And Signs Of Blue Lodge Masonry

ALAMA ZA FREEMASON.