Ridhiwan Kikwete kujenga kiwanda cha 'Tiles'
Mbunge wa Chalinze Ridhiwan Kikwete na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage
Ridhiwan Kikwete amesema kazi yake ni kutafsiri malengo mema aliyonayo Rais John Pombe Magufuli ya kujenga Tanzania ya viwanda kwa vitendo na kudai lengo kubwa la kujenga kiwanda hicho ni pamoja na kutoa ajira kwa vijana na wakina mama.
"Kitakapokamilika Kiwanda cha Tiles Twyford- Chalinze kinataraji kuajiri wafanyakazi rasmi 2000+ na Wasio Rasmi 4000+ na hii kazi ninayofanya ni kutafsiri malengo mema aliyonayo Rais na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa vitendo. Malengo makubwa ni kutoa ajira kwa vijana na wakina mama. Mungu anatusimamia tutafikia malengo tuliyojipangia" alisema Ridhiwan Kikwete.
Mbali na hilo Mh Ridhiwan Kikwete amedai kiwanda hicho kikikamilika malighafi zake za uendeshaji wa kiwanda hicho zitakuwa zikitoka Iringa, Kilimanjaro, Vikindu, Pugu, Morogoro na Tanga na kusema zaidi ya asilimia 90 ya malighafi zitakuwa zikitoka hapa hapa Tanzania.
"Malighafi Zitatoka Iringa, Kilimanjaro, Vikindu,Pugu, Morogoro, na Tanga. Yaani 90 percent inatoka Tanzania. kwa sasa akili, mwili na nguvu iko Chalinze. Inatakiwa nianze na Chalinze ndiyo nitabadili Tanzania kwa watu kuiga mfano wangu" alisisitiza Mh. Ridhiwan Kikwete.
Comments