Kiongozi wa Mexico akataa kulipia gharama za ujenzi wa ukuta

Rais wa Mexico anafikiria kufutilia mbali ziara aliyoipanga kuifanya Washington wiki ijayo kufuatia amri ya Rais Donald Trump kuwa ujenzi wa ukuta kati ya nchi hizo mbili uanze mara moja, amesema msemaji wa ngazi ya juu.


Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni kwa taifa Jumatano, Rais Enrique Pena Nieto amesema anasikitishwa na hakubaliani na uamuzi wa Marekani, na amerejea tena kusema  kwamba Mexico haitolipa gharama za ujenzi wa ukuta huo pamoja na Trump kutoa kauli hiyo.
“Mexico haiamini katika kuweka ukuta, “alisema rais huyo. “Nimesema mara nyingi, Mexico haitalipa gharama zozote za ujenzi wa ukuta.”

Pena Nieto hakusema moja kwa moja kuhusu safari yake, lakini akagusia kuwa atangojea ripoti kutoka kwa maafisa wa ngazi ya juu wa Mexico ambao hivi sasa wanakutana na uongozi wa Trump huko Washington.

Comments

Popular posts from this blog

Secret Masonic Handshakes, Passwords, Grips And Signs Of Blue Lodge Masonry

ALAMA ZA FREEMASON.