JAMMEH AELEKEA EQUATORIAL GUINEA



JAMMEH AELEKEA EQUATORIAL GUINEA.
Yahya Jammeh, aliyeondoka Gambia baada ya kutawala kwa miaka 22, ameondoka kutoka Guinea na kuelekea uhamishoni Equatorial Guinea.
Jammeh alikuwa amekubali kushindwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika Desemba lakini baadaye akakataa kuachia madaraka.
Aliondoka madarakani baada ya kushawishiwa na marais wa Guinea na Mauritania, huku majeshi ya muungano wa nchi za kanda ya Afrika Magharibi (Ecowas) yakitishia kumuondoa kwa nguvu.
Rais wa tume ya Ecowas Marcel de Souza amesema majeshi yaliyokuwa yameingia Gambia, sana kutoka Senegal, yataondoka sasa.
Hata hivyo, baadhi ya wanajeshi watasalia kwa muda.

Comments

Popular posts from this blog

Secret Masonic Handshakes, Passwords, Grips And Signs Of Blue Lodge Masonry

ALAMA ZA FREEMASON.